JIMBO KUU KATOLIKI – DAR ES SALAAM
PAROKIA YA MT. BONAVENTURA – KINYEREZI
‘‘Jubilee 2025 – Mahujaji wa Matumaini’’
MATANGAZO YA DOMINIKA YA 15 YA MWAKA C WA KANISA, TAREHE 13/07/2025
- UTANGULIZI
Leo ni Dominika ya 15 ya mwaka C wa Kanisa, pia ni Dominika ya pili ya zaka kiparokia. Dominika ijayo ni Dominika ya 16 ya mwaka C wa Kanisa. - USAFI NA USIMAMIZI
Tunazishukuru Jumuiya zilizofanya usafi jana na ambazo zinasimamia Misa za leo. Mungu awabariki sana.
Jumuiya za zamu Dominika ijayo ni kama ifuatavyo: –
1. Mt. Maurus, Misa ya I ,12:00 asubuhi
2. Mt. Gregory, Misa ya II , 2:00 asubuhi
3. Malaila Mkuu Raphael, Misa ya III, 4:00 asubuhi
4. Malaila Mkuu Gabriel, Misa ya IV, 10:00 jioni - SHEREHE YA SOMO WA PAROKIA NA KUMBUKIZI YA KUTABARUKU KANISA – 27/07/2025
Kutakuwa na sherehe ya somo wa Parokia yetu Mt. Bonaventura, Dominika ya tarehe 27/07/2025. Siku hiyo pia tufanya kumbukizi ya miaka minne tangu tulipotabaruku Kanisa letu. Sherehe hii itaadhimishwa kwa Misa Takatifu tu. Aidha, kama tulivyotangaza siku hiyo pia tutakuwa na ubatizo wa msamaha. Siku hiyo tutavaa vazi letu la Parokia, na vitenge vinapatikana kama bado huna vazi la Parokia. Pia siku hiyo tutavaa skafu tulizovaa siku ya Ekaristi, skafu zinapatikana kwa Tshs 5,000/= tu. - TANGAZO LA VIWAWA
Uongozi wa VIWAWA Parokia unawatangazia vijana kuwa Jumamosi ijayo tarehe 19/07/2025 ni siku ya fainali ya Kombe la Stela Maris na mchezo utafanyika katika viwanja vya JK Mnazi Mmoja, kuanzia saa kumi kamili jioni. Gharma za usafiri na muda wa kuondoka vitatumwa kwenye Jukwaa la Whatsapp la vijana. - MKUTANO WA HWP LEO BAADA YA MISA YA PILI
Kutakuwa na Mkutano wa HWP leo baada ya Misa ya pili. Wahusika ni Viongozi watano wa Kamati Tendaji ya Kigango, Kamati Tendaji za Kanda, na Wenyeviti wa VMJ ngazi ya Parokia. Wahusika wote wahudhurie Mkutano huu bila kukosa. - UCHAGUZI WA VIONGOZI WA JUMUIYA
Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya utaanza Jumamois ijayo tarehe 19/07/2025. Ratiba ya uchaguzi itatumwa katika majukwaa yetu ya Whatsapp. Tunaomba sana Jumuiya ambazo zitakuwa zinafanya uchaguzi, wazingatie kuwa siku ya uchaguzi mkutano utakuwa ni maalum kwa ajili ya uchaguzi. Aidha tunawasihi sana Wanajumuiya wote kuhakikisha wanahudhuria mikutano ya uchaguzi bila kukosa. - MATANGAZO YA NDOA
Mara ya pili
i. Martin Paul Mzonge kutoka Parokia ya Manyoni Singida, na Gemma Julius Nyerere kutoka Parokia ya Haubi Dodoma, wanatarajia kufunga ndoa tarehe 02/08/2025.
ii. Simon William Mahundi kutoka Parokia ya Namtumbo Songea, na Maria Benedicto Rafael, kutoka Parokia ya Kigoma, wanatarajia kufunga ndoa tarehe 30/08/2025.
iii. James Innocent Mkinga kutoka Parokia ya Mavanga Njombe, na Diana Bernard Msemo kutoka SDA Tanga, wanatarajia kufunga ndoa tarehe 28/08/2025.
Tuwaombee ili waweze kufikia Sakramenti hii ya Ndoa na mwenye kujua kizuizi chochote dhidi ya ndoa hizi au mojawapo atoe taarifa mapema kwa Baba Paroko.
Mwisho wa Matangazo – Tumsifu Yesu Kristo